Malaria ni ugonjwa unaoenezwa na mbu na kuambukizwa kwa binadamu
na wanyama wengine kupitia vimelea wa ugonjwa huu.
Malaria ni ugonjwa unaotishia maisha usababishwao na
vimelea waitwao plasmodium ambao huishi na kuzaliana wanapokuwa ndani ya damu. Ugonjwa
huu husambaa baada ya kuumwa na mbu ambaye huueneza kutoka mtu mmoja kwenda
mwingine. Baada ya vimelea kuingia kwenye damu huzaliana kisha kushambulia
chembe hai nyekundu za damu. Dalili huanza kuonekana siku chache baadae.
Na ugonjwa
huu hujiludia kama hautatibiwa kwa uhakika na kwa dawa sahihi.
Sababu za malaria
Malaria inasababishwa na kuumwa na mbu jike aitwae
Anopheles. Mara baada ya kukuuma mbu huyu huingiza vimelea wanaosababisha
maralia katika mfumo wa damu ambapo hukaa kwa muda fulani na kuelekea kwenye
ini ambako huzaliana na kusababisha ugonjwa.
Dalili za malaria
Dalili za malaria zinaweza kuwa katika makundi
mawili, maralia kali na isiyokali.
Malaria isiyo kali hutambulika wakati dalili zikiwepo, lakini hakuna ushahidi
wa maabara kuonesha wingi wa vimelea na uhalibifu wa viungo vya ndani ya mwili.
Watu wanaosumbuliwa na aina hii, wanaweza kupata malaria kali ikiwa mgonjwa
akiachwa bila kutibiwa.
Dalili hizi kawaida ni pamoja na homa, uchovu,
kichefuchefu, kutapika, maumivu ya kichwa, unyonge, maumivu ya misuli, baridi,
jasho,kuharisha.
Malaria kali inakuwa na ushahidi wa maabara na
husababisha baadhi ya viungo vya ndani ya mwili kuharibika. aina hii ina uwezo
wa kusababisha kifo kama ikiachwa bila kutibiwa. Kwa jumla dalili za maralia
kali ni:
• Homa na baridi kali
• kuharibika kwa mfumo wa fahamu
• degedege
• shida katika mfumo wa upumuaji
• upungufu wa damu
• Homa ya manjano na ini kutofanya kazi vizuri.
• Kutapika kila kitu
• Kupoteza hamu ya kula na kunyonya.
Matibabu kwa ugonjwa wa malaria
Matibabu ya ugonjwa wa malaria yanategemea kama ni
malaria ya kawaida au kali.
Katika matibabu ya maralia isiyokali dawa za kumeza
hutumika. Nazo ni kama vile;
• Artemether lumefantrine
• Dihydroartemisinin na Piperaquine
• Artemether sindano.
Katika matibabu ya maralia kali sindano ndizo
zinatumika.nazo ni kama vile
• Artesunate sindano
• sindano za Quinine.
Kumbuka; dawa za mara moja hazipaswi kutumiwa katika
matibabu ya maralia. mfano SP
Kukinga ugonjwa wa malaria
Malaria mara nyingi yaweza kukingwa na moja kati ya njia
hizi ambazo ni:
• Uelewa wa hatari
- kujua kama upo
katika hatari ya kupata ugonjwa wa malaria.
• kuzuia kung’atwa na mbu
- kuepuka
kuumwa na mbu kwa kutumia dawa ya mbu, kufunika mikono na miguu yako na kutumia
chandarua.
• Angalia kama unahitaji kutumia vidonge kuzuia malaria
- kama
utahitaji, hakikisha unapata dawa iliyosahihi na kwa kiwango sahihi, na
kumaliza dozi. Baadhi ya dawa zinazotumika ni;
• Atovaquone pamoja na proguanil
• Doxycycline
• Mefloquine.
• Chloroquine na proguanil
• Sulfadoxine na pyrimethamine.
• Uchunguzi wa maabara
- kutafuta ushauri na matibabu ya haraka kama
una dalili za malaria,
• kudhibiti mazaria ya mbu.
Matatizo yanayoweza kusababishwa na malaria.
Malaria ni ugonjwa mbaya ambao unaweza kusababisha kifo
kama mtu hata tambulika kuwa mgonjwa na kutibiwa kwa haraka, hasa kwa wanawake
wajawazito, watoto wachanga, wadogo na wazee.
Plasmodium falciparum ni vimelea vinavyosababisha zaidi maralia
kali na vifo kwa wagonjwa wa malaria.
Matatizo ya malaria kali yanaweza kutokea ndani ya masaa machache
au siku chache baada ya dalili ya kuonekana, hivyo ni muhimu kutafuta msaada wa
haraka wa matibabu haraka iwezekanavyo.
Upungufu wa damu.
uharibifu wa seli nyekundu za damu na vimelea vya malaria
inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu.
Upungufu wa damu hupelekea seli nyekundu za damu kutoweza
kubeba oksijeni ya kutosha kwenda kwenye misuli ya mwili,viungo na kuuacha
mwili dhaifu na usionanguvu.
Malaria ya ubongo
Mara chache malaria inaweza kuathiri ubongo. Hii
inajulikana kama malaria ya ubongo na inaweza kusababisha ubongo wako kuvimba,
wakati mwingine kusababisha uharibifu wa kudumu wa ubongo. Pia inaweza
kusababisha kifafa au kupoteza fahamu (kuzirai).
Matatizo mengine
Matatizo mengine ambayo yanaweza kutokea kutokana na
malaria kali ni pamoja na:
• kushindwa kwa ini kufanya kazi na homa ya manjano.
• mshtuko (kushuka ghafla kwa shinikizo la damu)
• uvimbe wa mapafu (mapafu kujaa maji)
• tatizo la mfumo wa upumuaji.
• kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu.
• kushindwa kwa figo kufanya kazi
• uvimbe na kupasuka kwa bandama
• upungufu wa maji mwilini
Malaria wakati wa ujauzito
Kama ukipata malaria wakati wa ujauzito, wewe na mtoto
wako mna hatari zaidi ya kupatwa na matatizo makubwa, kama vile:
• mtoto kuzaliwa mapema kabla ya muda.
• mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo.
• kupungua ukuaji wa mtoto tumboni.
• kuharibika kwa mimba.
• kifo cha mama.
kujifungua kichanga
kilichokufa
matibabu kipindi cha ujauzito.
katika miezi mitatu ya kwanza .
- · Quinine ndio dawa salama inayopendekezwa.
Katika miezi mitatu ya pili na mitatu ya mwisho .
- · ALU na Quinine ndio dawa salama zinazopendekezwa.
Kuzuia malaria kipindi cha ujauzito.
SP ni dawa chaguo la kwanza kuzuia maralia wakati wa
ujauzito .
No comments:
Post a Comment