Kwikwi ni tendo lisilo la hiyari linalohusisha kusinyaa kwa
gafla kwa sehemu inayotenganisha mapafu na tumbo (diaphragm)
na sehemu hii inahusika sana na upumuaji.
Kwikwi inaweza kujirudia mara kadhaa
kwa dakika.
Kwikwi ni tendo
lisilohiari ambalo pia huusisha mategemeo ya matendo mengine ya mwili. Mara tu baada ya kutokea mtegemeano huu husababisha msinyao wa nguvu wa sehemu hii
ikifuatiwa na kufunga kwa gafla kwa koo la hewa kwa tofauti ya sekunde chache
ikiambatana na kutoa sauti ya “hic”.
Kwikwi
inaweza kutokea katika hali ya kawaida au katika hali ya ugonjwa au pale mwili
unapopata tatizo. Katika hali ya kawaida kwikwi huisha yenyewe au kwa huduma za
asili za nyumbani. Matumizi ya dawa hutumika pale ambapo kwikwi imekaa kwa muda
mrefu bila kupotea.
Ishara na dalili za kwikwi
- Mara moja au mfululizo wa kusinyaa kwa diaphram wakati wa kupumua.
- Mtetemeko wa muda mfupi (chini ya nusu sekunde) usiotarajiwa wa mabega, tumbo, koo, au mwili.
- Hutokea na sauti ya "HUPP" au kama mtu kavuta hewa au chafya.
- Ikitokea huingilia mfumo wa upumuaji na huweza sababisha ghafla maumivu ya koo, kifua au tumbo.
- Katika baadhi ya matukio, kwikwi yaweza kuwa ni ishara ya tatizo fulani.
Sababu za kupatwa na kwikwi.
Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea mtu akapata kwikwi, lakini hakuna inayoonekana
kuwa sababu ya moja kwa moja ya kupelekea mtu kupata kwikwi. Na sababu hizi ni
kama zifuatazo.
- Kukohoa, kulia au kucheka kwa muda mrefu. Hii ni kawaida sana kwa watoto
- Kumeza hewa kupita kiasi
- kula kwa haraka. Kama mtu anakula chakula kwa haraka , anaweza kumeza hewa pamoja na chakula na kuishia kupata kwikwi.
- Hisia kali na za gafla kama vile hofu, wasiwasi, msisimko au furaha vinaweza kusababisha mtu kushikwa na kwikwi kwa mda mfupi au mrefu
- Njia yoyote inayoweza kusisimua diaphram ya mwili kama vile kula sana (hasa vyakula vya mafuta) mikate iliyo mikavu, vyakula vya pilipili au kunywa kupita kiasi (vinywaji vilivyosindikwa,pombe) vyaweza changia mtu kukabiliwa na kwikwi.
- Matumizi ya madawa yenye asili ya kulevya
- Uharibifu wa baadhi ya neva za fahamu za mwili.
- Baadhi ya dawa ambazo zinaweza kusababisha kiungulia pia zaweza sababisha kwikwi.
- Baadhi ya gesi zitumikazo katika kumbi za starehe kama vileo mfano noxious oxide
- Kupalalaizi au uvimbe kwenye ubongo na baadhi ya matatizo sugu ya matibabu kama vile kushindwa kwa figo kufanya kazi, maumivu ya ubongo na uti wa mgongo.
Kwikwi husababishwa na sababu mbalimbali katika mwili. Nani mara chache sana pale ambapo kwikwi huwa kama tatizo kubwa la kiafya.
Matibabu ya kwikwi.
Kwa kawaida kwikwi hutibiwa nyumbani
kupitia huduma za kawaida. Tiba za hospitali hutumika kwa tatizo linapokuwa
sugu.
Dawa zitumikazo zipo nyingi lakini hukuna dawa maarum kwa ajili ya kutibu kwikwi. Dawa nyingi zitumikazo ni kama vile
Dawa zitumikazo zipo nyingi lakini hukuna dawa maarum kwa ajili ya kutibu kwikwi. Dawa nyingi zitumikazo ni kama vile
- baclofen
- chlorpromazine
- metoclopramide
- Haloperidol
- gabapentin na
- zile zitumikazo kutibu vidonda vya tumbo.
Na kwa kwikwi inayosababishwa na tatizo fulani hutibiwa kwa kutibu tatizo sababishi.
Huduma binafsi na tiba asilia
Kuna matibabu mengi ya asili na imani za watu katika kutibu
kwikwi ikiwa ni pamoja na kusisimama kwa kutumia kichwa,
kunywa glasi ya maji kichwa-chini,
kumshtua mtu, kupumua katika mfuko,
na kula kijiko kikubwa
cha siagi ya karanga. Kuweka
sukari chini ya ulimi pia.
Pamoja na njia zote hizo kutumika moja kati ya tiba asilia iliyoonesha mafanikio ni ile ya kujizuia kupumua kwa kubana pumzi kwa muda ili kuzuia diaphram isifanye kazi kwa muda.
Pamoja na njia zote hizo kutumika moja kati ya tiba asilia iliyoonesha mafanikio ni ile ya kujizuia kupumua kwa kubana pumzi kwa muda ili kuzuia diaphram isifanye kazi kwa muda.
Hii nimeipenda... hili ni tatizo linatupata wengi.. atlast someone talked!
ReplyDeleteHii nimeipenda... hili ni tatizo linatupata wengi.. atlast someone talked!
ReplyDeleteSaf sana kwa elim nzur
ReplyDelete