Thursday, 20 August 2015

Vimelea Ngozi Maambukizi. (Fungal Skin Infection)


     Vimelea Ngozi Maambukizi.(fungal skin infection)
Husababishwa na aina mbalimbali za fungi, ikiwa ni pamoja na dermatophytes na yeasts. Fungi huvamia na kukua katika keratin iliyokufa. Keratin ni protini ambazo zinaunda ngozi yako, nywele na kucha. Kuna aina kadhaa tofauti ya maambukizi ya vimelea. Maambukizi hayo hugawanyika katika makundi tofauti kulingana na aina ya vimelea  vishiriki.

  SABABU ZAVIMELEA NGOZI MAAMBUKIZI.
Upo katika hatari ya kupatamaambukiziya vimeleangozi kama wewe
  • ni mwenye uzito uliokithili
  • hukaushi ngoziyakokikamilifubaada yakuoga
  • umegusana namtuau mnyamamwenye maambukiziya vimeleangozi
  •  umetumiavitumachafu vilivyokwisha tumiwa na mtu mwenye maambukiz kwa mfano nguo, taulo, nashuka.
  • hutembeabila viatu au ndalakatika maeneoya kuogea namabwawa
  • huvaa nguozinazobana kiasikwambahaziruhusujoto na jasho kupotea ama kukauka.
  • hutodhibitisukari yako kupanda kwa wale wenye ugonjwa wa kisukari
  • hivi karibuniumetumiadozi ya dawa za kuzuia au kuua vimelea(antibiotics)
  • ni mjamzito
  • unamfumo wa kingamwili ulio dhaifukutokana na magonjwamfanoVVU / UKIMWI

DALILI ZA VIMELEA NGOZI MAAMBUKIZI.
Dalili na muonekano wa maambukizi ya vimelea ngozi inategemea na aina ya kimelea aliesababisha maambukizi, pia itategemeana sehemu ya mwili ambayo imeathiriwa.

AINA ZA VIMELEA NGOZI MAAMBUKIZI.
• MAAMBUKIZI JUU YA NGOZI.
  1.  Nyungunyungu (tinea pedis)
Husababishwa na fangasi ambao hukua katika sehemu ya ngozi iliyo na joto na unyevunyevu pia,kama vile katikati ya vidole. Maambukizi ya vimelea hufanya ngozi yako iwashe,hafifu,nyekundu na yenye kubanduka. Ni pia husababisha nyufa nyeupe kuonekana hasa kati ya vidole na pande zoteza miguu, mara kwa mara husababisha Malengelenge. Unaweza patanyungunyungu kama wewe hutembea bila viatu katika mazingira yasio safi na yenye unyevunyevu, kama vile kuoga katika mabafu ya jumuiya na mabwawa ya kuogelea

 

 
Matubabu ya nyungunyungu.
• Dawa zitumikazo ni pamoja na clotrimazole, miconazole, Terbinafine, ketoconazole, butoconazole, naftine na tolnaftate.
• Hizi dawa hutumika juu ya ngozi ambazo hupakwa sehemu ya mwili iliyoathirika. Dawa za kupaka hufanya vizuri kuliko zile za kumeza.
• Pia kuna dawa zenye mchanganyiko wenye dawa tatu hizi hutoa msaadamkubwa kwenye ngozi wa kuzuia maambukizi mengine mbali na maambukizi ya vimelea ngozi vya fangasi.

            Jinsi ya kutumia dawa
• Safisha sehemu ya mwili iliyoathirika kwa maji safi kisha kausha na kitambaa safi au taulo,baada ya kukausha pakaa dawa kama utakavyo elekezwa namtoa dawa katika sehemu zilizoathirika. Hili lifanyike angalau mara mbili hadi tatu kwa siku kwa muda wa siku saba au mwezi.

        2. Maambukizi ya kucha (tinea unguium)

Kwa kawaida ukucha huanza kuathirika sehemu ya mbele na maambukizi husambaa hadi kwenye shina la ukucha, huchukua mda mrefu ukucha kuathirika. Maambukizi husababisha ukucha kupoteza rangi yake na wenye kubomoka au kapasuka.Misuli laini iliyondani ya kucha huvimba,hii husababisha ukucha pia kuvimba na kusababisha maumivu uvaapo viatu.Kucha za miguu ndizo huathirika zaidi kuliko zile za mikono.

 
 
Matibabu ya maaambukizi ya kucha.
• Dawa za kumeza ndizo zinazoweza kutibu kwa urahisi kuliko za kupaka. Daktari wako anaweza kuagiza upewe dawa za kumeza zenye uwezo wa kuua vimelea sababishi vya fungasi. Majaribio huonyesha matibabu yenye ufanisi ni yale yatumiayo dawa aina ya Terbinafine na itraconazole. Dawa hizi husaidiaukucha mpya kukua taratibu bila maambukizi na kuchukua sehemu iliyokuwa na maambukizi.
Matibabu haya kawaida huchukua muda wa wiki sita hadi kumi na mbili. Lakini huwezi kuona matokeo ya mwisho ya matibabu mpaka shina la ukucha litakapoanza kukua bila maambukizi. Inaweza kuchukua muda wa miezi minne au zaidi kuondokana na maambukizi.
Mafanikio ya matibabu kwa kutumia dawa hizi huonekana kuwa chini kwa watu wazima zaidi ya umri wa miaka 65. Matibabu huonyesha mafanikiozaidi pale dawa za kumeza zitakapo tumika kwa pamoja na zile za kupaka.
Dawa za kumeza zaweza leta madhara mengi kuanzia kwenye ngozi na kubwa zaidi zaweza sababisha uharibifu wa ini. Hivyo kwa mtu ambaye tayari ana tatizo la ini daktari ataangalia jinsi ya kumsaidia ili kuepuka athari zaidi.
• Pia kuna dawa nyingine ambayo ipo kwenye mfumo wa rangi yenyewe hupakwa kawaida kama rangi za kucha kwa ajili ya kuzuia maambukizi dawa hii huitwa ciclopirox.

     3.Mapunye au vibarango.(tinea corporis)

 Mara nyingi huathiri sehemu za wazi za mwili kama vile mikono,miguu,tumbo,mgongo au uso na husababisha ngozi kuwa nyekundu,vipele vidogovidogo viundavyo umbo la duara. Vibarango huenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine hasa kwa kugusana ama kuchangia vifaa.
 
 
 
 
Matibabu ya mapunye au vibarango
Ili kukabiliana na tatizo hili dawa za kupaka zenye uwezo wa kuua vimelea vya fangasi hutumika na katika hali ya  kawaida hutosha kutibu maambukizi. Dawa hizi hutumika moja kwa moja katika eneo la ngozi lililoathirika baada ya kuwa limesafishwa kwa maji safi na kukaushwa. Dawa zitumikazo ni pamoja na
   Ketoconazole cream
• clotrimazole cream
• miconazole cream
• Terbinafine cream
• tolfaftate cream
Mfamasia wako anaweza kukusaidia kuchagua dawa moja ambayo itakufaa zaidi.
Kama mapunye au vibarango ni vikubwa na ni vya mda mrefu kupelekea kutotibika kwa dawa za kupaka daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa za kumeza. Griseofulvin ni dawa ya kumeza inayoweza kuwa chaguo la kwanza baada ya dawa za kupaka kushindwa kutibu.
      4. Vibarango vya sehemu za siri (tinea cruris)
Pia hujulikanakitaaramu kama (Jockitch)kwa sababu hutokea zaidi kwavijana wa kiume. Hii ni kwa sababukorodanina sehemu ya juu ya mapaja vipo karibu hivyo kutengeneza mazingira hatarishi ya vimelea kukua na kuzalianakwa wingi.vinaweza piakuathiriwanawakeambao huvaa nguozinazobana sana.vinaweza kusababishamuwasho, vipele vya rangi nyekundukatika korodani naeneo lote la jirani.
 
Matibabu ya vibarango vya sehemu za siri
Tiba ya kwanza kabla ya dawa ni usafi wa hali ya juu katika sehemu hii ya mwili .dawa zitumikazo ni zile za kupaka na zilizo kwenye mfumo wa poda,dawa hupakwa mara mbili hadi tatu kwasiku baada ya kuoga na ni vizuri nywele zikaondolewa pia.
Baadhi ya dawa hizi ni:
Ketokonazoli, clotrimazole, miconazole, econazole, Terbinafine, tolnaftate, clotrimazole ikiwa pamoja na betamethasone.
.Ni muhimukukaa katika hali ya usafi kipindi chote cha tiba na baada ya tiba pia,ili maambukizi yasirudi kwa urahisi.
.Kama nafuu haita onekana na dalili kuendelea kwa zaidi ya majuma mawili basi daktari anaweza kushauri dawa za kumeza zitumike kwa pamoja na hizi za kupaka,dawa hizi ni kama vilefluconazole,Terbinafine.
    5.Vibarango vya kichwani  (Tine capitis)

Mara nyingi huwaathiri watoto ambao hawajafikia umri wa kubarehe . vinawezakuathirisehemu yoyote yakichwa chakolakinikwa kawaida huwekaalama za duara.Dalili zake ni sawa na zile za vibarango sehemu za sirina baada ya kutokea kichwa kitakuwa na mwonekano mbaya na kutakuwa na muwasho. Pia sehemu zenye vibarango zaweza kutunga usaa.Wakati wamaambukizinywele zakozinaweza kupotea na kuacha kipala lakini nywele huota tena baada ya matibabu
 

Matibabu ya vibarango wa kichwa

Dawa zinazotumika ni zile za kupaka(cream) na zile zilizo katika mfumo wa maji(shampoo). Lakini wakati mwingine dawa hizi haziwezi kutibu maambukizi haya kwasababu vimelea wanakuwa katika mashina ya nywele ambapo creams na shampoos haviwezi kufikia. Kwa hiyo dawa za kumeza zinatakiwa kutumika pamoja na shampoo au cream.

Shampoo au cream  inashauriwa kutumia mara mbili au mara tatu kwa siku, kwa muda wa wiki mbili hadi mwezi. Mfano wa dawa hizi huwa ni, selenium shampoo, ketoconazole shampoo. au Terbinafine cream.
Dawa  za vibarango za kunywa
• Griseofulvin hutumka kama chaguo la kwanza kwa matibabu ya vibarango vya kichwani  endepo cream na shampoo hazitotibu hii hutumika kwa muda wa wiki 8 mpaka 12
• Dawa zingine zinazotumika ni terbinafine,itraconazole,fluconazole.
 

 MAAMBUKIZI YA VIMELEA AINA YA YEAST.

  1.  Pityriasis versicolor (tinea versicolor)

Kama una maambukizi haya,sehemu za mgongo,sehemu za juu za mikono na kiwiliwili zitakuwa na alama za magamba,muwasho na ngozi kupoteza rangi yake ya asili na kuwa na rangi ya pinki,kahawia au nyekundu. Hii ni kawaida nyekundu, kahawia au rangi nyekundu. Kama una ngozi nyeusi, inaweza kupoteza uasili wa rangi yake.

 
 
 
 

Matibabu ya pytriasis versicolor
Baadhi ya dawa zitumikazo katika maambukizi haya ni zile za kupaka, na zingine ni dawa ambazo unaweza kumeza. Mifano ni pamoja na:
• fluconazole; vidonge
• itraconazole; vidonge,
• ketoconazole, cream, gelly au shampoo
Hata baada ya matibabu kufanikiwa, rangi ya ngozi yako yaweza kuchukua majuma kadhaa mpaka kurejea katika rangi yake ya kawaida. Pia  maambukizi yanaweza kujirudiakutokana na sababu mbalimbali,hivyo unashauriwa kutumia dawa tena kwa muda wa wiki moja hadi mbili baada ya matibabu ya awali.
 
      2. Fangasi wa mdomoni (candida albicans)
 
C. albicans ni aina ya fangasi ambaye kwa kawaida anaishi katika maeneo ya mdomo, tumbo, ngozi na ukeni kwa wanawake. Kwa kawaida huwa hasababishi tatizo lolote. Hata hivyo kama kiafya hauko vizuri, unamimba, umetumia dawa za kuua vimelea(antibiotics) au una ugonjwa wa kisukari,fangasi hawa  wanaweza kukua na kuzaliana na kusababisha dalili maambukizi ya fangasi za mdomoni. Maambukizi ya fangasi za mdomoni huonekana kama utando mweupe, ambao huacha alama nyekundu kama utakwanguliwa. Utando huu huenea sehemu ya ulimi,koo na kwenye pembe za mdomo.

 
Matibabu ya fangasi wa madomoni
Dawa nzuri zinazoweza kutumika katika maambukizi haya ni zile zilizoko katika mfumo wa maji. Na dawa zitumikazo mara kwa mara niNystatin, 1% gentianviolet. Kiasi kidogo cha dawa huwekwa mdomoni na kuachwa kwa muda kisha kutemwa. Hii hufanyika mara nne hadi sita kwa siku kwa muda usiopungua siku saba. Baadhi ya dawa za kumeza pia hutumika (kwa mfano,fluconazole).
Kinga ya vimelea ngozi maambukizi
Kuna hatuaunaweza kuchukua ilikupunguza hatari yakupatamaambukizi yangoziya vimeleanakuzuiamaambukizikueneza;
Hatua hizinikama ifuatavyo;
•Kaushangoziyako vizuribaadakuoga
•Safishasoksi, nguo na matandiko ya kitandamara kwa mara ilikuondoa vimelea.
•Vaaviatuvya wazi au plastiki katika maeneo yenye majimaji,sehemu za jumuiya, kama vile mabafunamabwawa ya kuogelea.
•Vaanguohuru zinazotosha vizuri na zilizotengenezwa kwa pamba au aina nyingine isiyotunza unyevu kwenye ngozi yako.
•usichangie taulo na vifaa vya kuchania nywele vinavyoweza kubeba vimelea.
•badili jozi ya viatu kila baaada ya siku mbili au tatu ili vipate kukauka.
•Kama unakisukari,hakikisha kiwango cha sukari ni kle kinachostahili kuwa katikadamu

Note; ni muhimu kutumia njia za usafi ili kukinga maambukizi kusambaa kwa watu wengine.
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Thursday, 13 August 2015

Malaria .



Malaria ni ugonjwa unaoenezwa na mbu na kuambukizwa kwa binadamu na wanyama wengine kupitia vimelea wa ugonjwa huu.
Malaria ni ugonjwa unaotishia maisha usababishwao na vimelea waitwao plasmodium ambao huishi na kuzaliana wanapokuwa ndani ya damu. Ugonjwa huu husambaa baada ya kuumwa na mbu ambaye huueneza kutoka mtu mmoja kwenda mwingine. Baada ya vimelea kuingia kwenye damu huzaliana kisha kushambulia chembe hai nyekundu za damu. Dalili huanza kuonekana siku chache baadae.
 Na ugonjwa huu hujiludia kama hautatibiwa kwa uhakika na kwa dawa sahihi.

Sababu za malaria

 
Malaria inasababishwa na kuumwa na mbu jike aitwae Anopheles. Mara baada ya kukuuma mbu huyu huingiza vimelea wanaosababisha maralia katika mfumo wa damu ambapo hukaa kwa muda fulani na kuelekea kwenye ini ambako huzaliana na kusababisha ugonjwa.


Dalili za malaria

 Dalili za malaria zinaweza kuwa katika makundi mawili, maralia kali  na isiyokali.
Malaria isiyo kali hutambulika  wakati dalili zikiwepo, lakini hakuna ushahidi wa maabara kuonesha wingi wa vimelea na uhalibifu wa viungo vya ndani ya mwili. Watu wanaosumbuliwa na aina hii, wanaweza kupata malaria kali ikiwa mgonjwa akiachwa bila kutibiwa.
Dalili hizi kawaida ni pamoja na homa, uchovu, kichefuchefu, kutapika, maumivu ya kichwa, unyonge, maumivu ya misuli, baridi, jasho,kuharisha.

Malaria kali inakuwa na ushahidi wa maabara na husababisha baadhi ya viungo vya ndani ya mwili kuharibika. aina hii ina uwezo wa kusababisha kifo kama ikiachwa bila kutibiwa. Kwa jumla dalili za maralia kali ni:
• Homa na baridi kali
• kuharibika kwa mfumo wa fahamu
• degedege
• shida katika mfumo wa upumuaji
• upungufu wa damu
• Homa ya manjano na ini kutofanya kazi vizuri.
• Kutapika kila kitu
• Kupoteza hamu ya kula na kunyonya.


Matibabu kwa ugonjwa wa malaria

Matibabu ya ugonjwa wa malaria yanategemea kama ni malaria ya kawaida au kali.
Katika matibabu ya maralia isiyokali dawa za kumeza hutumika. Nazo ni kama vile;

• Artemether lumefantrine
• Dihydroartemisinin na Piperaquine
• Artemether sindano.

Katika matibabu ya maralia kali sindano ndizo zinatumika.nazo ni kama vile

• Artesunate sindano
• sindano za Quinine.

Kumbuka;  dawa za mara moja hazipaswi kutumiwa katika matibabu ya maralia. mfano SP

Kukinga ugonjwa wa malaria

Malaria mara nyingi yaweza kukingwa na moja kati ya njia hizi ambazo ni:
• Uelewa wa hatari
   - kujua kama upo katika hatari ya kupata ugonjwa wa malaria.
• kuzuia kung’atwa na mbu
     - kuepuka kuumwa na mbu kwa kutumia dawa ya mbu, kufunika mikono na miguu yako na kutumia chandarua.
• Angalia kama unahitaji kutumia vidonge kuzuia malaria
   - kama utahitaji, hakikisha unapata dawa iliyosahihi na kwa kiwango sahihi, na kumaliza dozi. Baadhi ya dawa zinazotumika ni;

• Atovaquone pamoja na proguanil
• Doxycycline
• Mefloquine.
• Chloroquine na proguanil
• Sulfadoxine na pyrimethamine.

• Uchunguzi wa maabara
   - kutafuta ushauri na matibabu ya haraka kama una dalili za malaria,
• kudhibiti mazaria ya mbu.

Matatizo yanayoweza kusababishwa na malaria.

Malaria ni ugonjwa mbaya ambao unaweza kusababisha kifo kama mtu hata tambulika kuwa mgonjwa na kutibiwa kwa haraka, hasa kwa wanawake wajawazito, watoto wachanga, wadogo na wazee.
Plasmodium falciparum ni vimelea vinavyosababisha zaidi maralia kali na vifo kwa wagonjwa wa malaria.
Matatizo ya malaria kali yanaweza kutokea ndani ya masaa machache au siku chache baada ya dalili ya kuonekana, hivyo ni muhimu kutafuta msaada wa haraka wa matibabu haraka iwezekanavyo.

Upungufu wa damu.

uharibifu wa seli nyekundu za damu na vimelea vya malaria inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu.
Upungufu wa damu hupelekea seli nyekundu za damu kutoweza kubeba oksijeni ya kutosha kwenda kwenye misuli ya mwili,viungo na kuuacha mwili dhaifu na usionanguvu.

Malaria ya ubongo

Mara chache malaria inaweza kuathiri ubongo. Hii inajulikana kama malaria ya ubongo na inaweza kusababisha ubongo wako kuvimba, wakati mwingine kusababisha uharibifu wa kudumu wa ubongo. Pia inaweza kusababisha kifafa au kupoteza fahamu (kuzirai).

Matatizo mengine

Matatizo mengine ambayo yanaweza kutokea kutokana na malaria kali ni pamoja na:
• kushindwa kwa ini kufanya kazi na homa ya manjano.
• mshtuko (kushuka ghafla kwa shinikizo la damu)
• uvimbe wa mapafu (mapafu kujaa maji)
• tatizo la mfumo wa upumuaji.
• kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu.
• kushindwa kwa figo kufanya kazi
• uvimbe na kupasuka kwa bandama
• upungufu wa maji mwilini

Malaria wakati wa ujauzito

Kama ukipata malaria wakati wa ujauzito, wewe na mtoto wako mna hatari zaidi ya kupatwa na matatizo makubwa, kama vile:
• mtoto kuzaliwa mapema kabla ya muda.
• mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo.
• kupungua ukuaji wa mtoto tumboni.
• kuharibika kwa mimba.
• kifo cha mama.
  kujifungua kichanga kilichokufa



matibabu kipindi cha ujauzito.

katika miezi mitatu ya kwanza .
  • ·         Quinine ndio dawa salama inayopendekezwa.
Katika miezi mitatu ya pili na mitatu ya mwisho .
  • ·         ALU na Quinine ndio dawa salama zinazopendekezwa.

Kuzuia malaria kipindi cha ujauzito.

SP ni dawa chaguo la kwanza kuzuia maralia wakati wa ujauzito .